Dax ft. Maua - Safari (Prod_by_Ommyrunner)

Saturday, January 26, 20134comments

        Dax ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa MARA, wilaya ya TARIME kata ya BUHEMBA. Harakati za muziki alizianza takrbani miaka mitano iliyopita (yaani tangu 2007). Miaka mitatu ya kwanza(2007-2010) alishirikiana na wasanii kama  X I Z a.k.a. Bruno na G ZO a.k.a Hamza japo hakuwa amekamia kiviile, lakini miaka miwili ya mwisho(2011-2013) ndio alikuwa serious yaani Tayari kwa kufanya muziki wa biashara.(unaoeleweka kwa rika zote) 
        Mnamo July 2012 Dax aliweza kurekodi track yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la DAX maarufu kama TARIME STAND UP chini usimamizi wa Producer Ommyrunner aliyepika mdundo(BEAT) yake chini ya WE RUN ALL RUNNERS INC. na vocal zilijazwa katika studio za TALENT huko MUSOMA. Track hiyo ilimtambulisha vizuri kwani alikuwa style tofauti na alii-perform vizuri katika show mbalimbali mkoani Mara na hasa  ile ya SERENGETI FIESTA 2012.
       Mnamo January 2013,Dax aliweza kurekodi track yake ya pili iliyokwenda kwa jina la SAFARI aliyompa featuring mwanadada MAUA a.k.a MATTY MOE ambaye recently alivuma kwa Tracks kama MAPENZI NA DHIKI aliyoimba na Tundaman, RUMBA KALI na NIAMINI aliyeimba na CHID BENZ. Kutokana na utashi wa mistari ya DAX ndipo MAUA aliridhia kufanya CHORUS ya wimbo huu wa SAFARI uliokuwa produced by Ommyrunner katika studio za TALENT huko  MUSOMA.
       . Kwa hivyo, Support yako inahitajika sana kufanikisha hii safari ya mwanamuziki DAX. Kwa maelezo zaidi wasiliana nae kwa namba 0753174743 or 0656935153 au kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook: Dax Marl

Share this article :

+ comments + 4 comments

January 27, 2013 at 12:02 AM

..ngoma iko poa kinoma..!!

February 3, 2013 at 1:06 AM

cunajua digital joh

February 6, 2013 at 8:02 AM

good dud kaza buti utatoka

February 24, 2014 at 2:36 AM

we dogo nitafte kupitia 0768071538

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Ommy Runner | WE RUN ALL RUNNERS INC
Copyright © 2011. MASSTOWN MOVEMENTS - All Rights Reserved
Template Created by RUNNER INC Published by Ommyrunner
Proudly powered by MASSTOWN