

Harakati za kupinga Matumizi ya madawa ya kulevya na maambukizi ya virusi vya UKIMWI (drug abuse & HIV/AIDS Transmission) kwa kupitia burudani ya muziki zinazoendelea mkoani Mara, Jana zilikuwa maeneo ya Majita road Musoma mjini ambapo ziliudhuririwa na baadhi ya wasanii mkoani humo na wadau mbalimbali wa muziki.

Ilikuwa mida ya jioni ambapo show iliendeshwa na
MC Blez kutoka
RAP GENERATION huku DJBOX alikuwa
Ommyrunner pamoja na
Edeogratiz.Wasanii walohudhuria ni
Don XP, Ramawise, Kazo, Sayari, Willyson, Gwataman. Pia alikuwepo
Buddy Rhymes kama mdau na mwanaharakati wa muziki mkoani Mara.

Kili'happen sana kwani wakazi wa Kamunyonge na wengine wengi walijitokeza kusapoti harakati hizi.
Harakati hizi zilianzishwa kwa nguvu ya wasanii wenyewe mnamo 25/09/2014 katika maeneo ya SILVER SAND BEACH huku mbali na kupinga tabia hatarishi, zinalenga kukuza muziki wa mkoa wa Mara ilihali zimeanzia Musoma mjini.
Hivi ndivyo ilivyokuwa jana katika maeneo ya baruti
Post a Comment